Rukirabashaija amesema hakua katika hali ya usalama alipokua Afrika akihofia kwamba anaweza kurudishwa nyumbani kutokana na hali kwamba viongozi wa kimabavu barani humo hushirikiana pamoja.
Umoja wa Ulaya ni miongoni mwa washirika walioomba uchunguzi wa kina kuhusu vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Uganda.
Rukirabashaija aliyeachiliwa kwa dhamana amesema kwamba aliondoka Uganda kupitia Rwanda kwa mgu na kusafiri kupitia nchi ya tatu kabla ya kuwasili Ujerumani.
Wakili Eron Kiiza amesema bila kutoa maelezo zaidi kwamba baada ya hapo shirika la Umoja wa mataifa linalohudumia wakimbizi ( UNHCR) ndilo lilimusaidia kufika Ujerumani.