Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 16:22

Mwanahabari wa Marekani auwawa Afghanistan


Mwandishi wa habari, David Gilkey.
Mwandishi wa habari, David Gilkey.

Mwandishi wa habari mkongwe wa Marekani na mkalimani wake wa Afghanistan waliripotiwa kuuwawa nchini Afghanistan Jumapili, baada ya kushambuliwa waktiwa kisafiri na kikosi cha kijeshi cha Afghanistan katika jimbo la kusini la Helmand.

'National Public Radio' ya Marekani iliwatambua waandishi hao kuwa ni mpiga picha David Gilkey na mkalimani Zabihullah Tammana. Waandishi wengine katika msafara huo walinusurika.

Hakukuwa na taarifa nyingine mara moja na juu ya ukubwa wa kikosi cha kijeshi au kama kulikuwa na majeruhi wengine.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, ambaye yuko Beijing kwa sasa amesema shambulizi hili la kutisha ni ukumbusho wa hatari inayoendelea kuwakumba watu wa Afghanistan na moyo wa waandishi wa habari jasiri.

XS
SM
MD
LG