Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 22, 2023 Local time: 17:58

Mwandishi mwingine auwawa Uganda


Rais wa Uganda Yoweri Museveni (Jul 2010 file photo)

Polisi wa Uganda wanasema mwandishi mmoja wa radio amepigwa hadi kufariki dunia

Polisi wa Uganda wanasema mwandishi mmoja wa radio amepigwa hadi kufariki dunia, akiwa ni mwandishi wa pili kuuwawa katika nchi hiyo chini ya wiki moja.

Polisi walisema kuwa kundi la watu likiwa na vyuma lilimshambulia Dickson Ssentongo aliyekuwa na umri wa miaka 29 wakati akienda kazini Prime Radio Jumatatu.

Shambulizi hilo lilitokea huko Mukono magharibi mwa mji mkuu Kampala maafisa wanasema kuwa mauaji yake yanahusishwa na siasa za nchi hiyo.

Jumamosi iliyopita Paul Kiggundu ripota wa radio Top alishambuliwa na kundi la waendesha pikipiki wakati akijaribu kupiga filam watu hao wakati wakichoma nyumba ya mtu anayeshukiwa kuuwa dereva mwenzao wa boda boda.

XS
SM
MD
LG