Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 07:26

Mwandishi mwingine auawa Somalia


Raia wa Somalia wakisikiliza habari kwenye radio.
Raia wa Somalia wakisikiliza habari kwenye radio.

Mkurugenzi wa kituo cha radio auwawa na watu wenye silaha Somalia akiwa ni wa pili katika kipindi cha mwezi mmoja.

Watu wenye silaha nchini Somalia walimpiga risasi na kumuuwa mkurugenzi wa kituo cha radio ambacho kilifungwa na kundi la wanamgambo la alshabab mwaka 2010. Mashahidi waliiambia Sauti ya Amerika kwamba Abubakar Hassan Kadaf alishambuliwa na watu wawili wakiwa na bastola Jumanne usiku alipokuwa akirudi nyumbani kwake Mogadishu. Alithibitishwa kuaga dunia kwenye hospitali ya mji huo. Haikubainika mara moja ni nani aliyemwua. Muungano wa waislam Somalia ulilaani mara moja mauaji hayo na kusema kwamba Kadaf alikuwa ni mkurugenzi wa pili kuuawa Mogadishu katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita. January 28 watu wenye silaha walimuuwa Hassan Osman Abdi mkurugenzi wa Radio Shabelle.

XS
SM
MD
LG