Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 09:47

Mwandishi maarufu wa Blog, Vietnam afikishwa mahakamani


Mwandishi maarufu wa blog, Nguyen Huu Vinh.
Mwandishi maarufu wa blog, Nguyen Huu Vinh.

Mwandishi maarufu wa blog na msaidizi wake nchini Vietnam walifikishwa mahakamani mjini Hanoi mapema leo kwa kesi ya mashitaka ya kuchapisha Makala inayoikosoa serikali.

Nguyen Huu Vinh na Nguyen Thi Minh Thuy wamekuwa wakishikiliwa kutoka walipokamatwa mwaka 2014. Waendesha mashitaka walisema mfululizo wa makala zilichapishwa na Nguyen Huu Vihn katika blog yake, makala ambazo zilikuwa na habari zisizo za ukweli, maoni ya upande mmoja juu ya chama tawala cha Kikomonisti ambazo zilichochea watu kutokuwa na imani na viongozi wake.

Vihn vilevile anatambulika kama Anh Ba Sam alitengeneza blog inayoitwa “Ba Sam” mwaka 2007. Blog hiyo ilionganishwa na chombo cha habari cha serikali vilevile blog nyingine za wanaharakati.

XS
SM
MD
LG