Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 13, 2024 Local time: 10:49

Mwandishi maarufu wa soka Marekani Grant Wahl afariki dunia Doha


Picha ya Selfie ya Grant Wahl ambaye alidai kuwa alikamatwa kwa muda alipojaribu kuingia uwanjani akiwa amevalia shati la upinde wa mvua kuunga mkono jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja huko Al Rayyan, Qatar.Novemba 21, 2022
Picha ya Selfie ya Grant Wahl ambaye alidai kuwa alikamatwa kwa muda alipojaribu kuingia uwanjani akiwa amevalia shati la upinde wa mvua kuunga mkono jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja huko Al Rayyan, Qatar.Novemba 21, 2022

Mwanahabari maarufu wa soka wa Marekani Grant Wahl alifariki dunia ghafla siku ya Ijumaa baada ya kuzimia alipokuwa akifuatilia mechi ya Kombe la Dunia kati ya Argentina na Uholanzi nchini Qatar, wakala wake alisema.

Chama cha soka nchini Marekani kilisema "kimesikitishwa na habari juu ya kifo cha Wahl. Mkewe alijibu taarifa ya chama cha soka Marekani kwenye Twitter, akisema "ameshtushwa sana ".

Waandalizi wa Kombe la Dunia la Qatar, Kamati Kuu ya usimamizi wa kombe la dunia Supreme Committee for Delivery and Legacy (SC) walitoa heshima kubwa kwa upendo mkubwa wa mpira wa miguu wa Wahl na kutoa rambirambi kwa familia yake, marafiki na wafanyakazi wenzake wa vyombo vya habari.

Wahl, mwandishi mkongwe wa gazeti la Sports Illustrated ambaye alihamia kwenye jukwaa la mtandaoni la Substack, alilioanzisha alikuwa akitweet kuhusu mechi ya Uholanzi na Argentina mapema Ijumaa.

Wakala wake, Tim Scanlan, aliiambia Reuters kwamba Wahl alionekana kuugua mwanzoni mwa muda wa ziada kwenye mechi hiyo ya robo fainali.

Scanlan alisema majaribio yalifanywa kuokoa maisha ya Wahl kwenye chumba cha waandishi wa habari kabla ya kupelekwa katika hospitali ya eneo hilo, ambapo alithibitishwa kuwa amefariki dunia.

Chanzo cha habari ni Shirika la Habari la Reuters

XS
SM
MD
LG