Tovuti hiyo inachunguzwa kwa kunyakua kazi ya mamlaka ya uchaguzi, ambayo inasema Rais Nicolas Maduro alishinda uchaguzi wa Julai 28 lakini haijachapisha matokeo ya kina.
Mamlaka ya kitaifa ya uchaguzi nchini Venezuela na mahakama yake kuu imesema Maduro ndiye mshindi wa uchaguzi huo kwa zaidi ya nusu ya kura, lakini hesabu zilizotangazwa na upinzani zinaonyesha ushindi mkubwa wa Gonzalez.
Upinzani, baadhi ya nchi za Magharibi na mashirika ya kimataifa kama jopo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamesema upigaji kura haukuwa wa uwazi na kutaka kuchapishwa kwa hesabu kamili, huku baadhi yao wakikemea udanganyifu.
Forum