Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 10, 2024 Local time: 18:51

Mwanasiasa wa upinzani ameuawa Msumbiji


Wapiga kura nchini Msumbiji OCT 9 2024
Wapiga kura nchini Msumbiji OCT 9 2024

Watu waliokuwa na bunduki wamempiga risasi na kumuua mwanasiasa wa upinzani nchini Msumbiji.

Chama cha PODEMOS kimesema kwamba Elvino Dias, wakili wake na mshauri wa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha upinzani Venancio Mondlane, na msemaji wa chama wameuawa katika mashambulizi ya risasi.

Watu hao walikuwa wanatumia usafiri wa magari mawili.

Mauaji hayo yametokea katika mji mkuu wa Maputo, jana Ijumaa usiku. Waliouwa walipokuwa wakijitayarisha kuwasilisha kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi huu.

Uchaguzi huo umekumbwa na madai ya wizi wa kura na unyanyasaji wa wanasiasa wa upinzani.

Forum

XS
SM
MD
LG