Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 22, 2023 Local time: 17:50

Mwanasiasa wa Nigeria afunguliwa mashitaka Uingereza kwa ulanguzi wa viungo


Ike Ekweremadu na mke wake kwenye picha za maktaba

Polisi nchini Uingereza wamewafungulia mashtaka mwanasiasa mmoja wa Nigeria,pamoja na mkewe , kwa kupanga njama za kumpeleka mtoto mwenye umri wa miaka 15 hadi Uingereza ili kumtoa sehemu za vioungo vya.

Ike Ekweremadu, mwenye umri wa miaka 60, Senata wa jimbo, pamoja na wakili Beatrice Nwanneka Ekweremadu mwenye umri wa miaka 55, wanakabiliwa na mashtaka ya kupanga safari ya mtu mwingine kwa lengo la kumtoa baadhi ya viungo muhimu vya mwili wake.

Washukiwa hao wawili wamefikishwa katika mahakama ya Uxbridge, magharibi mwa London.

Wamethibitisha kwamba wanaishi nchini Nigeria. Wamezuiliwa na polisi hadi kusikilizwa kesi yao inayotarajiwa kuanza July tarehe 7.

Polisi wamesema kwamba mtoto aliyekuwa amesafirishwa kwa ajili ya kutolewa viungo muhimu vya mwili amechukuliwa na yupo salama.

Waongoza mashitaka wanawalaumu kwa kupeleka David Nwamini Ukpo mwenye umri wa miaka 15 hadi Uingereza kwa nia ya kumtoa figo ya kusiadia binti yao.

Ekweremadi na mke wake pia wanashutumiwa kudanganya kwamba kijana huyo alikuwa na umri wa miaka 21. Haijabainia iwapo Ukpo alifahamu kwamba alipelekwa Uingereza kwa nia ya kumtoa figo.

Polisi wamesema kwamba walianza kufanya uchunguzi baada ya kupata taarifa za ulanguzi wa binadamu, mnamo mwezi May.

Ike Ekweremadu alikuwa amealikwa na chuo kikuu cha Lincolin, kaskazini mwa Uingereza kama profesa aliye kwenye ziara ya mda.

XS
SM
MD
LG