Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:23

Mwanamke wa kwanza kugombea urais Niger.


Ramani ya Niger
Ramani ya Niger

Uchaguzi ujao wa urais nchini Niger utajumuisha mgombea mwanamke kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo.

Uchaguzi ujao wa urais nchini Niger utajumuisha mgombea mwanamke kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo. Waziri wa zamani wa utamaduni Mariama Bayard alitangaza kuwa atagombea urais katika uchaguzi huo.

Bayard alisema atapambana ili kuiinua Niger kutoka katika mzozo wa kisiasa na kiuchumi na atakuwa mtetezi wa watu masikini nchini humo. Uchaguzi huo unalengo la kurejesha utawala wa kiraia huko Niger baada ya mapinduzi ya kijeshi mapema mwaka huu.

Niger ni moja ya mataifa masikini sana duniani ikiwa imekumbwa na upungufu wa chakula, hasa katika eneo lake la jangwa la sahara. Uchaguzi wa urais umepangwa kufanyika Januari 3 na marudio ya upigaji kura Januari 14 kama itakuwa muhimu.

XS
SM
MD
LG