Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 21:49

Mwanamke aliyetekwa nyara Kenya aachiwa huru


Kikosi cha kundi la wanamgambo wa Alshabab.
Kikosi cha kundi la wanamgambo wa Alshabab.

Mwanamke aliyetekwanyara aachiwa huruV na vyombo vya habari vya Uingereza vimeeleza familia ya Tebutt ililipa fidia.

Wateka nyara nchini Somalia wamemwachia huru mwanamke mmoja wa Kiingereza kutoka kwenye eneo la mapumziko katika pwani ya Kenya ambaye wamekuwa wakimshikilia kwa zaidi ya miezi 6 iliyopita .

Mashahidi wanasema Judith Rebbutt aliachiwa huru kutoka katika mkoa wa Addado nchini Somalia hii Jumatano na kupelekwa kwa ndege hadi Nairobi. Maafisa wa Uingereza na Somalia walithibitisha kuachiwa kwake.

Vyombo vya habari vya Uingereza vimeeleza familia ya Tebutt ililipa fidia ili aachiwe huru.

Watu wenye silaha walimteka nyara Tebutt na kumuuwa mume wake David Septemba mwaka jana , muda mfupi baada ya kuwasili kwenye eneo la mapumziko la Kiwayu Safari Village kiasi cha kilometa 40 kusini mwa mpaka wa Somalia na Kenya. Walikuwa ndio wageni pekee wa eneo hilo la mapumziko kwa wakati huo.

XS
SM
MD
LG