Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 13:41

Mwanamke aliyerusha mfuko kwenye uzio wa White House akamatwa


Sehemu iliyofungwa ya uzio wa White House, Washington DC.
Sehemu iliyofungwa ya uzio wa White House, Washington DC.

White House ilifungwa kwa muda siku ya Jumatatu baada ya mwanamke mmoja asiyejulikana kurusha mfuko uliokuwa na vitu vya chuma kwenye uzio wa jengo upande wa kaskazini, maafisa kutoka idara ya usalama walisema.

Wahudumu wa dharura wakiwemo kitengo cha kujibu vifaa vya hatari waliitwa kufanya uchunguzi. Maafisa wanasema kifaa cha kugundua vitu vya hatari vilionesha mfuko huo haukuwa na hatari yeyote.

Kufungwa kwa baadhi ya eneo la White House kulitokea saa kadhaa baada ya Rais Barack Obama kurejea White House kutoka kwenye makaburi ya kitaifa ya Arlington yaliopo jimbo la Virginia ambako alitoa hotuba ya siku ya mashujaa.

Mwanamke huyo anayeshukiwa kutupa mfuko kwenye uzio wa White House alikamatwa na kuchukuliwa bila ya vurugu. Maafisa walisema familia ya Obama haikuwa katika hatari yoyote.

XS
SM
MD
LG