Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 02:40

Mshukiwa wa mauaji Bangladesh akamatwa


Members of Bangladesh Police Detective Branch escort Sumon Hossain Patwari in Dhaka, Bangladesh, Thursday, June 16, 2016.
Members of Bangladesh Police Detective Branch escort Sumon Hossain Patwari in Dhaka, Bangladesh, Thursday, June 16, 2016.

Mwanamgambo wa itikadi kali za kislamu ambaye anashukiwa kumshambulia mchapishaji mwaka jana amekamatwa Jumatano jioni kwa kile polisi walichokielezea kuwa ni hatua muhimu katika kufanikisha uchunguzi kuhusu hali ya sasa ya mashambulizi mabaya yanayozuka nchini Bangladesh.

Sumon Hossain Patwari, mwenye umri wa miaka 20, anashutumiwa kuhusika na mauaji ya kikatili ya mchapishaji Ahmed Rashid Tutul na waandishi wengine wawili ambao walipigwa risasi na watu watatu katika ofisi ya uchapishaji ya Shidhdhoswar, mjini Dhaka mwezi Oktoba, mwaka jana.

Polisi wanasema Patwari ni mwanachama wa kundi la Ansarullah Bangla Team ('ABT') - kikundi ya wanamgambo cha Bangladesh kilichopigwa marufuku.

Mkuu wa sasa wa kikosi cha kupambana na ugaidi, Monirul Islam, amewaambia wanahabari kwamba mtu huyo amekiri alimvamia mchapishaji huyo Tutul wakati wa shambulizi mara tatu.

XS
SM
MD
LG