Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 23:03

Mwanajeshi wa Rwanda akamatwa Uganda


Rais wa Rwanda Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul Kagame

Mwanajeshi wa Rwana aliyetorokea Uganda, Sgt Major Robert Kabera amekamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi mkali jijini Kampala, Uganda.

Kabera alitoroka Rwanda Novemba 2020 akidai kwamba alikuwa anaandamwa na serikali ya Rwanda.

Amekamatwa katika mtaa wa Masanafu, jijini Kampala.

Kabera, ambaye anaishi Uganda kama mkimbizi, amesema kwamba wanajeshi walivamia nyumbani kwake na kufanya msako “wakitafuta bunduki.”

Walioshuhudia msako huo wamesema hakuna bunduki imepatikana katika msako huo.

Vyombo vya habari vya Uganda vinaripoti kwamba kuna mipango ya kumrudisha Rwanda japo mawakili wake wanatarajiwa kufika mahakamani kupinga hatua hiyo.

Serikali ya Rwanda imesema kwamba Kabera anachunguzwa na jeshi la Rwanda kwa madai ya kufanya mapenzi na msichana wa familia yake mwenye umri wa miaka 15 mnamo mwezi Novemba tarehe 21 mwaka uliopita.

Kabera amekanusha madai hayo akisema mnamo mwezi Novemba, alikuwa tayari nchini Uganda akiishi kama mkimbizi kinyume na madai kwamba likuwa Rwanda.

Alimbia gazeti la Daily Monitor mnamo mwaka 2020 kwamba masaibu yake yanatokana na uhusiano wake na familia ya marehemu Fred Rwigema, kamanda wa Rwanda Patriotic front, ambaye aliuawa mwezi Oktoba mwaka 1990 wakati kundi lake lilijaribu kuvamia Rwanda kwa mara ya kwanza.

Kabera vile vile anadai kwamba serikali ya Rwanda inashuku kwamba anajua siri za aliyekuwa mwanamziki marehemu Kizito Mihigo aliyepatikana kama amefariki katika kizuizi cha polisi.

XS
SM
MD
LG