Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 05, 2023 Local time: 00:21

Mwanajeshi wa Russia ahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kumua raia wa Ukraine


Mwanajeshi wa Russia Sajenti Vadim Shishimarin, aonekana mahakamani wakati kesi dhidi yake ikisikilizwa mjini Kyiv, May 18, 2022. Picha ya AP.

Mwanajeshi wa Russia ambaye alikiri kumuua raia wa Ukraine amehukumiwa kifungo cha maisha jela Jumatatu na mahakama ya Ukraine, licha ya ishara kuwa Kremlin nayo inaweza kuwafikisha mahakamani baadhi ya wapiganaji wa Ukraine waliokomatwa kwenye uwanja wa mapambano.

Hata hivyo, baadhi ya maafisa wa Russia wanaendelea kuelezea hadharani upinzani wao dhidi ya vita vya Russia nchini Ukraine, mwanadiplomasia mkongwe amejiuzulu na kutuma barua ya kujiuzulu kwa wanadiplomasia wenzake wa kigeni ambamo alisema kuhusu uvamizi huo “ Sijawahi kuwa na aibu kwa nchi yangu kama Februari 24.”

Katika kesi ya kwanza kuhusu uhalifu wa kivita ndani ya Ukraine, mwanajeshi wa Russia mwenye cheo cha Sajenti Vadim Shishimarin, mwenye umri wa miaka 21, amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kumua mzee mwenye umri wa miaka 62 kwa kumpiga risasi kichwani katika kijiji kimoja cha mji wa kaskazini mashariki wa Summy katika siku za mwanzo za vita.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG