Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 27, 2025 Local time: 12:10

Mwanaharakati Hong Kong ashitakiwa


Chombo cha kupambana na rushwa cha Hong Kong, Jumanne kimemshtaki mtaalamu wa program za Kompyuta, Man Wing-fung, mwenye umri wa miaka 38.

Mashitaka hayo yanahusu kuchochea watu kutopiga kura, jambo ambalo lilifanywa ni kinyume cha sheria mwaka 2021 ikiwa sehemu ya juhudi za serekali kukandamiza wakosoaji.

Tume huru ya kupambana na rushwa ya Hong Kong (ICAC) pia ilituma maombi ya kutaka jaji atoe hati ya kukamatwa kwa Wong Sai-chak mwenye umri wa miaka 45, mtoa maoni ya kisiasa mzaliwa wa Hong Kong anayejulikana mtandaoni kama Martin Oei anayeishi Ujerumani.

ICAC imemshutumu mtu huyo kwa kuchapisha tena maoni yake mwishoni mwa Oktoba, na Novemba, ambayo yalichochea watu kususia uchaguzi wa wilaya wa Hong Kong wa 2023.

Chapisho lake lilikuwa na video ambayo Wong, alitoa wito kwa wakazi wa Hong Kong kutopiga kura katika kile alichoiambia VOA kuwa uchaguzi usio wa haki.

Forum

XS
SM
MD
LG