Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 05:28

Mwanaharakati apigwa risasi Burundi.


Askari wa Burundi washika doria kwenye mitaa ya Bujumbura.
Askari wa Burundi washika doria kwenye mitaa ya Bujumbura.

Mwanaharakati maarufu amepigwa risasi na kujeruhiwa vibaya katika mji mkuu Bujumbura siku moja baada ya generali wa juu wa kijeshi kushambuliwa na kuuwawa.

Viongozi wa kiraia nchini Burundi wanasema mwanaharakati maarufu amepigwa risasi na kujeruhiwa vibaya katika mji mkuu Bujumbura siku moja baada ya generali wa juu wa kijeshi kushambuliwa na kuuwawa.

Viongozi wa kiraia wamesema Pierre Claver Mbonimpya ambaye anaongoza jumuiya ya ulinzi wa haki za binadamu na wafungwa, alipigwa risasi na mtu aliyekuwa kwenye pikipiki wakati akienda nyumbani Jumatatu.

Wamesema alipelekwa katika hospitali moja ya ndani nchini humo akiwa na majeraha mabaya.

Mbonimpoya alimkosoa hadharani rais Pierre Nkurunzinza kuhusu maamuzi yake yaliyokuwa na utata ya kugombea muhula wa tatu wa uongozi na aliwahi kufungwa jela kwa sababu ya shughuli zake za uanaharakati.

Haijafahamika nani aliyefanya shambulizi hilo.

Burundi imetumbukia katika mzozo wa kisiasa tangu mwezi Aprili baada ya rais Pierre Nkurunzinza kutangaza nia yake ya kugombea muhula wa tatu wa uongozi.

XS
SM
MD
LG