Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 18:33

Mwanahabari wa Marekani azuiliwa Congo


Wapiganaji kutoka kundi la uasi la M23 kwenye mji wa Karuba mashariki mwa Congo. Picha ya maktaba
Wapiganaji kutoka kundi la uasi la M23 kwenye mji wa Karuba mashariki mwa Congo. Picha ya maktaba

Afisa wa ngazi ya juu wa serikali  ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya congo amesema Jumapili kwamba idara ya kijasusi ya nchi hiyo , imemkamata  mwanahabari wa Marekani Starvos Nicolas Niarchos kwa tuhuma za kuwasiliana na makundi yenye silaha kusini mashariki mwa taifa hilo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, asasi za kiraia kama vile RECN zimekaririwa na vyombo vya habari vya zikisema kwamba Niarchos pamoja na mwandishi wa habari wa Congo walikamatwa Jumatano katika mji wa kusini mashariki wa Lubumbashi, na kisha kupelekwa mji mkuu wa Kinshasa.

Afisa wa ngazi juu wa sserikali ambaye hakutaka kutajwa jina lake ameithibitisha AFP Jumapili kwamba Niarchos anashikiliwa na idara ya kijasusi ya ANR mjini Kinshasa. Afisa huyo ameongeza kusema kwamba Niarchos mwenye umri wa miaka 33, na ambaye huandikia magazeti ya Marekani ya The Nation na The New Yorker, amekuwa akiwasiliana na makundi yenye silaha likiwemo kundi la Bakata Katanga.

Mwaka 2017, wataalam wawili kutoka Marekani na Sweden waliokuwa wametumwa na Umoja wa mataifa kuchunguza ghasia kwenye eneo la Kasai nchini humo walitekwa nyara na kisha kuuwawa na watu wasiojulikana.

XS
SM
MD
LG