Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 21, 2024 Local time: 06:14

Mwanafunzi amjeruhi mwenzake kwa risasi Florida


Wanafunzi wakifarijiana baada ya shambulizi la kutumia silaha katika shule ya sekondari ya Forest mjini Ocala, Florida, Aprili 20, 2018.
Wanafunzi wakifarijiana baada ya shambulizi la kutumia silaha katika shule ya sekondari ya Forest mjini Ocala, Florida, Aprili 20, 2018.

Mwanafunzi wa sekondari upande wa kusini mashariki mwa jimbo la Florida nchini Marekani amempiga risasi na kumjeruhi mwanafunzi wa darasa lake Ijumaa, na maelfu ya wanafunzi nchi nzima siku hiyo hiyo walitoka madarasani kuomboleza mauaji ya shule ya sekondari ambayo yalitokea miongo miwili iliyopita.

Katika shambulizi hilo lililotokea Ijumaa katika shule ya sekondari, huko mji wa Ocala, Florida, mkuu wa polisi wa kaunti ya Marion amesema kuwa mtu anayeshukiwa kuwa alishambulia amewekwa ndani.

Maandamano hayo ya kitaifa yameandaliwa na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Marjory Stoneman Douglas huko mji Parkland, Florida, ambako wanafunzi 17 na mfanyakazi mmoja waliuwawa na mwanafunzi wa zamani Februari 14.

Mauaji hayo ya Parkland yaliibua kampeni nchi nzima kwa ajili ya kushinikiza kuwepo sheria kali zaidi za udhibiti silaha. Maandamano hayo yanajumuisha maandamano ya hivi karibuni yaliyofanyika Washington na miji mingine kote nchini Marekani.

Wanafunzi wa shule ya sekondari mjini Washington wamepanga kuandamana kuelekea White House na pia hadi Bunge la Marekani baadae Ijumaa wakitaka wabunge kuchukua hatua ili kupitisha sheria kali zaidi za udhibiti wa silaha.

Wanafunzi hao wanaungana na wenzao kutoka shule zaidi ya 2600 na taasisi nyingine nchini kote ambao walitoka madarasani, wengi wao wakiwa wamevaa nguo rangi ya machungwa ambayo imekuwa ikinasibishwa na harakati za kudhibiti silaha.

Shughuli hiyo ya Ijumaa ni kwa ajili ya kumbukumbu ya Aprili 20, 1999 ambapo wanafunzi katika shule ya sekondari ya Columbine huko magharibi mwa jimbo la Colorado, wanafunzi wawili waliokuwa ndani ya eneo la shule , waliwauwa wanafunzi wenzao 12 na mwalimu mmoja kabla ya kujiuwa.

XS
SM
MD
LG