Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 14, 2024 Local time: 10:54

Mwanafunzi afunguliwa mashtaka ya kuuwa shuleni Texas


Nicole Auzston, kulia, na mtoto wake Branden, 17, mwanafunzi wa shule ya sekondari ya awali ambaye alikuwa shuleni wakati wa shambulizi hilo la bunduki wakiwa na huzuni wakati walipokutana katika kituo cha kuwaunganisha wazazi na watoto wao baada ya mauaji hayo katika shule ya sekondari ya Fe High, Mei 18, 2018.
Nicole Auzston, kulia, na mtoto wake Branden, 17, mwanafunzi wa shule ya sekondari ya awali ambaye alikuwa shuleni wakati wa shambulizi hilo la bunduki wakiwa na huzuni wakati walipokutana katika kituo cha kuwaunganisha wazazi na watoto wao baada ya mauaji hayo katika shule ya sekondari ya Fe High, Mei 18, 2018.

Maafisa wa polisi katika mji wa Texas Ijumaa wamemfungulia mashtaka kijana mwenye umri ya miaka 17 kwa kosa la kuuwa katika shambulizi la bunduki lililouwa watu 10, wengi wao wakiwa wanafunzi, katika shule ya sekondari ya Santa Fe, Texas.

Watu wengine kumi walijeruhiwa katika shambulizi hilo, akiwemo afisa wa polisi anayelinda shule hiyo ambaye alikuwa mtu wa kwanza kukabiliana na mshukiwa huyo.

Wanafunzi wamesema mshambuliaji huyo aliyekuwa na silaha, ametambuliwa na vyombo vya usalama kama Dimitrios Pagourtzis, mwanafunzi wa shule ya sekondari ya awali, ambaye alishambulia shule hiyo kwa bunduki kabla ya saa mbili asubuhi.

Majina ya waliouwawa katika shambulizi hilo yanaendelea kutolewa, na kati yao ni mwalimu mbadala na mwanafunzi wa kigeni aliyekuwa katika programu ya shule hiyo ya kubadilishana wanafunzi.

Cynthia Tisdale, mwalimu, alikuwa kati ya wale waliouwawa Ijumaa asubuhi katika Shule ya Sekondari ya Santa Fe, familia yake imethibitisha.

Tisdale alikuwa katika ndoa yake na mumewe kwa miaka 40 na walikuwa tayari wana watoto watatu na wajukuu wanane, mpwa wao wa kike Leia Olinde amesema.

Sabika Sheikh, akiwa katika programu ya kubadilishana wanafunzi kutoka Pakistan, naye aliuwawa, Ubalozi wa Pakistan mjini Washington umethibitisha hilo.

Jumuiya ya Pakistan inayosimamia kuifanya Houston kuwa Bora Zaidi umesema katika ukurasa wake wa Facebook kuwa Sabika alikuwa katika maandalizi ya kwenda Pakistan kwa ajili ya sikukuu ya Eid al-Fitr, mapumziko ya siku tatu ambayo yanaadhimisha kumalizika kwa mwezi wa Ramadhan katika dini ya Uislam.

XS
SM
MD
LG