Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:41

Mwakilishi wa  Umoja wa Mataifa : suluhu ya kisiasa Myanmar si rahisi

Mfuasi akionyesha picha ya kiongozi wa zamani Aung San Suu Kyi wakati wa maandamano ya kuadhimisha miaka miwili ya kutwaa mamlaka ya kijeshi ambayo yaliondoa serikali yake nje ya Ubalozi wa Myanmar mjini Bangkok, Thailand, Februari 1, 2023. AP

Mwakilishi wa  Umoja wa Mataifa kwa Myanmar alisema Alhamisi kwamba uwezekano wa kupatikana kwa suluhu ya kisiasa kwa nchi hiyo kuchukuliwa na jeshi bado  si rahisi.

Kwa kuwa pande zote mbili zina nia ya kushinda kwa nguvu hakuna matarajio ya suluhu iliyojadiliwa Mjumbe Maalum Noeleen Heyzer aliliambia Baraza Kuu katika mukhtasari wa hali hiyo.

Myanmar imekumbwa na machafuko na vurugu tangu jeshi lilipokataa matokeo ya uchaguzi wa Novemba 2020 na kupindua serikali ya kiraia iliyochaguliwa kidemokrasia Februari mosi 2021.

Tangu wakati huo mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema maelfu ya raia wakiwemo watoto wengi wameuawa na kukamatwa katika msako mkali.

Jeshi pia limemkamata na kumhukumu kiongozi ambaye hajachaguliwa Aung San Suu Kyi, Rais U Win Myint na maafisa wengine wa ngazi za juu kutoka chama kilichoondolewa madarakani cha National League for Democracy.

XS
SM
MD
LG