Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 17:03

Mwakilishi wa AU afukuzwa Somalia


Mwakilishi wa umoja wa Afrika nchini Somalia Francisco Madeira. PICHA: AFP
Mwakilishi wa umoja wa Afrika nchini Somalia Francisco Madeira. PICHA: AFP

Waziri mkuu wa Somalia amemfukuza mwakilishi wa umoja wa Afrika nchini humo kwa kile kimetajwa kama kufanya vitu ambavyo havilingani na hadhi yake.

Hata hivyo, rais wa Somalia amekataa amri ya waziri wake mkuu na kuonyesha hali ya kutokuwepo uelewano kati ya viongozi hao wakuu wa serikali ya Somalia.

Ofisi ya waziri mkuu Mohamed Hussein Roble, imesema kwamba mwakilishi wa umoja wa Afrika, balozi Francisco Madeira, ni lazima aondoke nchini humo ndani ya saa 48.

Taarifa ya Ofisi ya waziri mkuu haikutoa maelezo zaidi kuhusu hatua ya kumfukuza Madeira.

Madeira, ambaye ni raia wa Msumbiji, hajajibu shutuma hizo.

Amri hiyo ya kumfukuza Madeira ineonekana kuvuruga zaidi mvutano wa kisiasa kati ya Roble na rais Mohamed Abdullahi Mohamed, na kupelekea kuwepo wasiwasi kwamba ukaathiri kampeni ya kupambana na waasi wa Alhsabaab nchini humo.

Wanajeshi wa muungano wa Afrika unasaidia serikali ya Somalia kupambana na waasi wa Al-shabaab.

XS
SM
MD
LG