Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 21:37

Mwakilishi asiye wa kisiasa amealikwa kuzungumza kwenye mkutano wa ASEAN mwezi huu


Bendera za nchi wanachama wa ASEAN
Bendera za nchi wanachama wa ASEAN

Uamuzi ulifikiwa na mawaziri wa mambo ya nje kutoka Jumuiya ya mataifa ya kusini mashariki mwa Asia (ASEAN) katika mkutano wa dharura Ijumaa usiku inaashiria hatua nadra ya ujasiri kwa umoja unaotekelezwa na makubaliano ambao kijadi unapendelea sera ya ushiriki na kutokuingiliwa

Nchi za kusini mashariki mwa Asia zitamkaribisha mwakilishi ambaye sio wa kisiasa kutoka Myanmar kwenye mkutano wa kikanda mwezi huu kutoa mtazamo usio wa kawaida kwa kiongozi wa jeshi aliyeongoza mapinduzi dhidi ya serikali iliyochaguliwa ya kiraia hapo Februari.

Uamuzi ulifikiwa na mawaziri wa mambo ya nje kutoka Jumuiya ya mataifa ya kusini mashariki mwa Asia (ASEAN) katika mkutano wa dharura Ijumaa usiku inaashiria hatua nadra ya ujasiri kwa umoja unaotekelezwa na makubaliano ambao kijadi unapendelea sera ya ushiriki na kutokuingiliwa.

Wizara ya mambo ya nje ya Singapore ilisema Jumamosi hatua ya kumtenga mkuu wa kikosi kinachodhibiti serikali Min Aung Hlaing, ilikuwa uamuzi mgumu lakini muhimu wa kuhimili uaminifu wa ASEAN.

Taarifa hiyo ilitaja ukosefu wa maendeleo yaliyofanywa kwenye ramani ya mipango ya kurejesha amani nchini Myanmar ambapo kikosi cha jeshi kinachotawala kilikubaliana na ASEAN hapo mwezi April. Msemaji wa serikali ya jeshi la Myanmar alilaumu uingiliaji wa kigeni kwa uamuzi huo.

XS
SM
MD
LG