Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 21:31

Mvutano wazuka ndani ya serikali ya Italia


Naibu Waziri Mkuu wa Italia Matteo Salvini akihutubia baraza la seneti Italia
Naibu Waziri Mkuu wa Italia Matteo Salvini akihutubia baraza la seneti Italia

Kiongozi wa chama kinachotawala nchini Italia, ambaye ni naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani Matteo Salvini, ameitisha uchaguzi mapema baada ya kutangaza kwamba serikali ya muungano haiwezi kuendelea kufanya kazi.

Hatua yake inafuatia miezi kadhaa ya mikwaruzano ndani ya serikali hiyo ya miezi 14, kati ya chama cha siasa kali za mrengo wa Kulia na washirika wake.

Hali ya mgogoro serikalini, imeiweka Italia, ya tatu kwa uchumi mkubwa katika nchi zinazotumia sarafu ya Euro, katika hali ngumu ya kisiasa, isiyoweza kutabirika.

Katika taarifa, Salvini amesema amemwambia Waziri Mkuu Giuseppe Conte, ambaye sio mwanachama wa muungano wowote unaounda serikali, kwamba muungano wa serikali umevunjika na kwamba kwa haraka, anastahili kuwapa mamlaka wapiga kura kufanya maamuzi.

Alhamisi, Salvini alihutubia wafuasi wake katika mji wa Pecara, pwani ya Adriatic, na kusema mda umewadia kwa wapiga kura wa Italia kufanya uamuzi.

Waziri Mkuu huyo ambaye ameshiriki katika duru kadhaa za mazungumzo kutafuta suluhu la mgogoro serikalini, hata hivyo amesema Sio wajibu wa Salvini kuitisha kikao cha bunge, wala kuweka mda wa kusuluhisha mgogoro wa kisiasa, na kwamba viongozi wengine wanastahili kuingilia kati.

Conte, amemtaka Salvini kujieleza ni kwa nini anataka serikali kuvunjwa.

Bunge la Italy, ambalo sasa limo katika mapumziko, huenda likarejelea vikao vyake wiki ijayo ili kuchukua hatua muhimu.

Kabla ya serikali kuvunjwa, bunge linastahili kupiga kura ya kutokuwa na Imani na serikali, na waziri mkuu kujiuzulu.

XS
SM
MD
LG