Milio mipya ya mizinga inatishia rasi ya Korea na kupelekea maonyo mapya wakati mvutano ukiongezeka kati ya Korea kaskazini na kusini.
Wakazi katika kisiwa cha Korea kusini cha Yeonpyong waliripoti kusikia milio ya makombora kutoka Korea kaskazini siku ya Ijuma.
Maafisa wa kijeshi wa Korea Kusini wamesema hakuna makombora yaliofyetuliwa kwenye eneo lao lakini tukio hilo limetokea siku tatu tu baada ya mashambulizi ya makombora ya Korea kaskazini kwenye kisiwa hicho , kuuwa wanajeshi wawili na raia wawili na kujeruhi wengine 18.