Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 14:52

Mvutano waongezeka Ivory Coast kabla ya Uchaguzi mkuu Jumamosi


 Alassane Ouattara supporters in Abidjan - 3e mandat ADO
Alassane Ouattara supporters in Abidjan - 3e mandat ADO

Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo ameonya kwamba taifa hilo la Afrika magharibi linaweza kuingia kwenye machafuko makubwa iwapo wagombea kwenye uchaguzi wa jumamosi, hawatosuluhisha mvutano uliosababisha maandamano ya vurugu na wito wa upinzani wa kususia uchaguzi.

Washambuliaji wasiojulikana walichoma moto magari kadha na kuvamia makazi katika mji wa biashara wa Abidjan jumatatu, polisi ilisema.

Wakati jana ilikua siku ya mwisho ya kampeni kabla ya uchaguzi, Gbagbo amesema amehisi ni vizuri kuzungumza na waandishi wa habari tangu akamatwe mwaka 2011 kutokana na jukumu lake katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, vilivyochochewa na kutokubali kwamba alishindwa na Ouattara.

Mwaka uliopita, mahakama ya kimataifa ya uhalifu(ICC) ilimuachilia na kumuondolea Gbagbo mashtaka ya uhalifu wa kivita yanayohusiana na mzozo uliofwatia uchaguzi wa 2010, ambapo watu elfu 3 waliuwawa.

“Tunakoelekea ni kwenye machafuko makubwa, ndio maana nazungumza”, Gbagbo ameiambia televijeni ya ufaransa TV5 Monde.

Watu 30 wameuwawa katika vurugu tangu mwezi Agosti, wakati rais Ouattara alipotangaza kuwania muhula wa tatu, hatua ambayo upinzani unasema unakiuka katiba ya nchi.

Wapinzani wake wawili, rais wa zamani Henri Konan Bedie na waziri mkuu wa zamani Affi N’Guessan waliomba wafuasi wao kuzuia uchaguzi usifanyike.

Imetayarishwa na Patrick Nduwimana, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG