Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 19:49

Mvutano wa Sudan wakwama juu ya Abyei


Wananchi wa Sudan
Wananchi wa Sudan

Wajumbe kutoka Kaskazini na Kusini mwa Sudan wanatarajiwa kufanya mikutano mjini Addis Ababa katiuka juhudi za kuafikiana juu ya Abyei

Wajumbe kutoka Kaskazini na Kusini mwa Sudan wanatarajiwa kufanya mikutano mjini Addiss Ababa Jumatatu, katika juhudi za kuafikiana juu ya suala la tete la eneo lenye utajiri wa mafuta la Abyei. Mhusika wa tatu kwenye majadiliano hayo, Marekani, inazihimiza pande hizo mbili kufikia makubaliano ambayo yatawezesha eneo la Abyei kuamua ikiwa linataka kujiunga na upande wa Kaskazini au ule wa Kusini.

Majadiliano yanawaleta pamoja wawakilishi kutoka chama tawala cha Sudan cha National Congress party, na chama cha Sudan Peoples’ Liberation Movement SPLA.

Pande hizo mbili zilifanya duru ya kwanza ya mazungumzo Jumapili jioni, pamoja na mjumbe maalum wa Marekani kwa Sudan, Scott Gration, vilevile mwanadiplomasia za siku nyingi wa Marekani ambaye pia ni mpatanishi Princeton Lyman, pamoja na mwenyeji wa mazungumzo hayo waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi.

Msemaji wa ubalozi wa Marekani Alyson Grunder, anasema pande hizo mbili zinatarajiwa kuwa tayari kutatua tofauti juu ya masharti ya kura ya maoni kuamua wajibu wa Abyei, ikiwa upande wa Kusini utapiga kura kuwa huru katika kura ya maoni ya Januari mwakani.

XS
SM
MD
LG