Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 10, 2025 Local time: 03:26

Mvutano kati ya wanajeshi na polisi waongezeka Somalia


Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed

Wabunge wa Somalia wamemchagua spika mpya leo alhamisi huku kukiwepo hali ya mivutano kati ya wanajeshi wa kulinda amani wa umoja wa Afrika AU, na polisi.

Mivutano hiyo inadhihirisha mpasuko uliopo katika vyombo vya usalama vya Somalia, kutokana na kucheleweshwa kwa uchaguzi.

Jumatano, polisi watiifu kwa rais Mohamed Abdullahi Mohamed, maarufu kama Farmaajo, waliwazuia wabunge waliokuwa wanajaribu kuingia kwenye ukumbi wa uwanja wa ndege ambapo uchaguzi ulikuwa unafanyika, wakiwaambia kwamba uchaguzi huo ulikuwa umeahirishwa.

Wakati huo huo, waziri mkuu Mohamed Hussein Roble, ambaye amekuwa katika mzozo wa madaraka na rais Mohamed kwa miezi mingi, alikuwa amewaamuru walinda usalama kulinda sehemu uchaguzi ulikokuwa unafanyika ili kuwaruhusu wabunge kushiriki zoezi hilo, hatua ambayo imepelekea kutokea msukumano kati ya maafisa wa usalama.

Baadaye, wabunge wamemchagua Sheikh Adan Mohamed Nur kama spika wa baraza kuu la bunge.

Uchaguzi wa spika ni muhimu sana katika kuunda serikali mpya ambayo lazima iwe imeundwa ifikapo May 17 ili Somalia iendelee kupata msaada wa fedha kutoka shirika la kimataifa la fedha duniani IMF.

XS
SM
MD
LG