Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 06:18

Idara ya hali ya hewa India yawapa wana vijiji matumaini ya msimu mzuri wa mvua


Wakazi wa kijiji cha Mayong nchini India walioathiriwa na mvua za Monsoon wakitembea kwenye daraja la muda.
Wakazi wa kijiji cha Mayong nchini India walioathiriwa na mvua za Monsoon wakitembea kwenye daraja la muda.

Wakati India ikikabiliana na hali ngumu ya kilimo na upungufu wa maji kutokana na miaka miwili ya kiangazi, utabiri wa kutokea kwa mvua kubwa za msimu kumeleta matumaini kwamba hali itabadilika hasa mashambani.

Tangazo hilo kutoka Idara ya Hali ya Hewa ya India limeeleza kuna matarajio ya mvua ya zaidi ya asilimia 6 kuliko kawaida. Taarifa imetolewa wakati idara hiyo ikiwa imetuma treni iliyobeba lita nusu milioni za maji kuelekea kwenye eneo lililoathiriwa zaidi na ukame la Latur katika jimbo la magharibi la Maharashtra.

Arun Kulkarni, ambaye ni mkazi kutoka eneo hilo, anasema kuwa mabomba ya maji yalikauka mwezi mmoja uliopita kutokana na kukauka kwa bwawa lililokuwa likitegemewa. Anasema wenye uwezo wanakwenda kutafuta maji hadi kilomita 15 huku wasio na uwezo wakitumia saa nyingi kutafuta angalau lita moja ya maji.

XS
SM
MD
LG