Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 05, 2024 Local time: 06:35

Marekani na Canada zajadili mustakbali wa kibiashara


Rais Donald Trump na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau wakiwa White House
Rais Donald Trump na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau wakiwa White House

Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, wanao tofautiana maoni yao juu ya biashara na uhamiaji, wamekutana Jumatatu kwa mara ya kwanza huko White House, Washington DC.

Biashara kati ya nchi hizo mbili jirani zinatarajiwa kutawala ajenda yao, wakati kiongozi mpya wa Marekani akitafuta jinsi ya kurejesha mazungumzo au kufuta mkataba wa soko huria la Amerika ya Kaskazini wa 1994 unao zihusisha Marekani, Canada na Mexico, ili kuurekebisha uwe na maslahi zaidi kwa Marekani.

Mahusiano ya kibiashara ni muhimu kwa pande zote -- Ottawa na Washington. Asilimia 75 ya bidhaa za Canada zinauzwa Marekani na asilimia 18 ya bidhaa za Marekani zinauzwa Canada.

Ratiba ya Trudeau ya ziara yake ya siku moja inahusisha mazungumzo yake na Spika wa Bunge Paul Ryan na kiongozi wa waliowengi katika Baraza la Seneti Mitch McConnell.

Trudeau na Trump wana mtizazmo tofauti kabisa kuhusu uhamiaji. Kiongozi wa Canada amewapokea wakimbizi wa Syria 40,000.

Wakati huo huo, Trump amekabiliwa na mapambano ya kisheria kwa amri yake ya kiutendaji ya kuzuia kwa muda wasafiri wanaotaka kuingia Marekani kutoka nchi saba zenye waislamu wengi zenye historia ya mashambulizi ya kigaidi na kusitisha programu ya wakimbizi nchini.

XS
SM
MD
LG