Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 17:23

Museveni aitembelea Somalia

Rais wa Uganda Yoweri Museveni(R), akiwa na Rais wa Somalia Sheikh Sharif Ahmed(L)
Rais wa Uganda Yoweri Museveni(R), akiwa na Rais wa Somalia Sheikh Sharif Ahmed(L)

Rais wa Uganda Yoweri Museveni,amefanya ziara fupi Jumapili huko Somalia, nchi yenye mapigano na nadra kutembelewa na wakuu wa nchi za nje.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni,amefanya ziara fupi Jumapili huko Somalia, nchi yenye mapigano na nadra kutembelewa na wakuu wa nchi za nje.

Maafisa wanasema bwana Museveni alizungumzia usalama na masuala mengine na rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, waziri mkuu mpya Mohammed Abdullahi Mohamed na maafisa wengine kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mogadishu.

Msemaji wa jeshi la Umoja wa Afrika huko Mogadishu alisema bwana Museveni alipeleka ujumbe wa mshikamano kwa watu wa Somalia. Baadae alitembelea kambi za walinda amani wa Umoja wa Afrika kabla ya kuondoka nchini humo.

Uganda na Burundi zina wanajeshi 7,200 wa Umoja wa Afrika wanaoisaidia serikali ya Somalia inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa yenye udhibiti mdogo wa madaraka kwenye maeneo muhimu ya mji mkuu.

Makundi ya wanamgambo ya al-Shabab na Hizbul Islam yanadhibiti sehemu kubwa ya nchi, yakiwemo maeneo makubwa ya mogadishu, na kuibana serikali katika eneo dogo linalolindwa na wanajeshi wa Umoja wa Afrika.

XS
SM
MD
LG