Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 03:44

Museveni ashiriki mdahalo wa urais Uganda


Rais wa Uganda Yoweri Museveni,kushoto, na mmoja wa wapinzani wake Kizza Besigye.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni,kushoto, na mmoja wa wapinzani wake Kizza Besigye.

Rais Yoweri Museveni wa Uganda anashiriki katika mdahalo wa wagombea urais unaofanyika mjini Kampala, Uganda Jumamosi na kushirikisha wagombea wanane wa urais nchini humo.

Huu ni mdahalo wa pili wa wagombea urais lakini ni mara ya kwanza kwa Rais Museveni kushiriki zikiwa zimebaki siku tano kabla ya uchaguzi Februari 18.

Wagombea wametumia muda mrefu kuzungumzia maswala ya usalama katika eneo zima la maziwa makuu na wakati fulani mabishano makali yalizuka baina ya wagombea wawili wakuu Rais Yoweri Museveni na Kizza Besigye ambaye ni mpinzani wake mkuu kwa miaka mingi.

Wakati fulani baadhi ya wagombea walilalamika kuwa mdahalo umegeuka kuwa uwanja wa Museveni na Besigye kujadili ugomvi wao ambao umedumu kwa muda mrefu.

XS
SM
MD
LG