Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 16:38

Museveni ashtumu Besigye na vyombo vya habari


Kiongozi wa Upinzani Kizza Besigye akihutubia mkutano wa hadhara Kampala, Januari 24, 2012
Kiongozi wa Upinzani Kizza Besigye akihutubia mkutano wa hadhara Kampala, Januari 24, 2012

Museveni alaumu Besigye kwa matatizo ya Uganda

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametoa lawama kali kwa wapinzani wake wa kisiasa na vyombo vya habari huku akisema mafanikio ya kiuchumi nchini humo yametokana na juhudi zake. Katika hotuba kwa Waganda juu ya hali ya kitaifa wakati wa ufunguzi wa kikao cha pili cha bunge mjini Kampala Alhamis, Bw. Museveni alisifu maendeleo ya kiuchumi nchini mwake na kuelezea juu ya gharama ya maisha na uhaba wa ajira. Lakini pia alilalamika vikali juu ya mpinzani wake mkuu Kizza Besigye, akimshtumu kwa kuiwakilisha vibaya Uganda na kwa kuwavunja moyo watalii na hivyo kuinyima Uganda dola zinazotokana na watalii. Rais Museveni alisema ukiukwaji wa kanuni za kisheria unaofanywa na Besigye umeongeza tatizo la uhaba wa dola za kimarekani na hivyo kushusha hadhi ya shilingi ya Uganda. Aliwapongeza maafisa wa polisi kwa kuchukua hatua dhidi ya Besigye na njama zake za kile alichosema ni jaribio la kupindua katiba ya Uganda. Bw. Museveni pia alishutumu vyombo vya habari akisema vimejaa ufisadi, haviwajibiki wala kuzingatia maadili. Alionya kuwa vyombo vya habari vitakavyoshindwa kuweka mizani katika ripoti zake, zitatokomea, na kuvikumbusha kuwa mamlaka ya kutoa leseni kwa vyombo hivyo ni la serikali.

XS
SM
MD
LG