Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:39

Museveni aanza ziara ya siku tatu Tanzania


Rais Yoweri Museveni, kulia, na Rais Samia Suluhu Hassan. (Photo by - / Presidential Press Unit of Uganda / AFP) /
Rais Yoweri Museveni, kulia, na Rais Samia Suluhu Hassan. (Photo by - / Presidential Press Unit of Uganda / AFP) /

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni yuko  nchini Tanzania  kuhudhuria mkutano wa mafuta na gesi na pia kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan. 

Kwa mujibu wa wasaidizi wake, Rais Museveni atahutubia katika ufunguzi wakati wa mdahalo wa sekta binafsi ulioandaliwa kujadili fursa zinazoletwa na mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki lenye urefu wa kilomita 1,445.

Nchi hizo mbili mwezi Aprili mwaka 2021 zilisaini mikataba ya serikali, mikataba ya ubia (kwa ajili ya kampuni ya ujenzi wa bomba la mafuta ) na mikataba ya tozo, mikataba mitatu itakayowezesha ujenzi wa bomba hilo la mafuta kwa kushirikiana na kampuni ya Total ya Ufaransa na kampuni ya CNOOC ya China.

Lakini mradi huo bado unakabiliwa na matatizo ya kifedha baada ya wakopeshaji wa Ulaya kujiondoa kuufadhili mradi.

Mradi wa EACOP unatarajiwa kutengeneza ajira 5,000 za moja kwa moja na zaidi ya 20,000 zisizo za moja kwa moja.

Rais Museveni yuko kwenye ziara ya siku tatu nchini humo na anatarajiwa kujadili masuala mbali mbali ya ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili.

XS
SM
MD
LG