Jafar Panahi, (62) na ambaye filamu zake zimewasisimua wakosoaji na kushinda tuzo nyingi kimataifa, alitoa taarifa akisema alitarajia kuanza kukataa chakula au dawa kuanzia Jumatano, kupinga vitendo visivyo vya kisheria na kinyama vya vyombo vya mahakama na usalama.
Yeye ni miongoni mwa wasanii kadhaa wa Iran, wanamichezo na watu wengine mashuhuri ambao wamezuiliwa baada ya kuikosoa serekali ya Iran.
Kukamatwa kwa watu kama hao kumeongezeka tangu maandamano ya kitaifa yalipozuka Septemba baada ya kifo cha msichana mmoja akiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Facebook Forum