Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 14:19

Mume amnyonga mkewe na kujiua Uganda


Polisi nchini Uganda inachunguza tukio ambalo mtu anadaiwa kumuua mkewe kwa kumnyonga na baadae kujiua kwa kujinyonga.

Afisa upelelezi wa kituo cha Manispaa ya Kasese Peter Tindyebwa amesema tukio hilo lilitokea katika majira ya usiku wa saa sita Jumanne katika eneo la Kikonzo, Kata ya Railway katika eneo la katikati ya manispaa.

Maiti hizo zilitambuliwa kuwa ni Francis Nitware na mkewe Annet Nkunzimana wote wakazi wa kijiji cha Kabuga huko Karusandara kaunti ndogo. Walikuwa wanaishi katika nyumba yakukodi.

Polisi imesema tukio hilo ni matokeo ya ugomvi uliokuwepo kati ya familia hiyo. Wanafamilia hao waliishi pamoja kwa takriban karibu miaka kumi lakini hawakuwahi kupata mtoto.

Kwa mujibu wa Melesi Kabugho, jirani, mwanamume huyu alikuwa akimtuhumu mkewe kwa kuwa na mahusiano ya nje ya ndoa na wanaume wengine mjini hapo..

Kamanda wa Polisi wa Rwenzori Richard Ecega ameliambia gazeti la Daily Monitor kuwa mauaji yanayotokana na manyanyaso ya kinyumbani katika wilaya hiyo ni asilimia 70 ya kesi ambazo zinaripotiwa. Tindyebwa amesema kesi za manyanyaso ya kinyumbani zimefikia asilimia 60 katika manispaa hiyo.

Hadi jioni, miili hiyo ya marehemu ilikuwa bado iko kwenye kituo cha Afya cha Manispaa ya Kasese ikisubiri kufanyiwa uchunguzi.

XS
SM
MD
LG