Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 29, 2022 Local time: 17:32

Muhtasari wa Uchaguzi Mkuu Kenya (2017)


Rais Uhuru Kenyatta

Utaratibu wa kuhesabu kura za ushindi ni kwamba mgombea anayeibuka kidedea kwenye nafasi ya urais lazima awe na zaidi ya asilimia hamsini (50%) ya kura zote.

Mfumo wa Kumpata Rais wa Kitaifa

Wakati huo huo mgombea huyo ni lazima awe walau na asilimia ishirini na tano (25%) kwenye majimbo walau 24 ambapo Kenya ina majimbo 47.Hii ni moja ya hatua ambazo taifa la Kenya limechukua kukabiliana na tatizo la siasa za ukabila. Wachambuzi wa kisiasa wanasema kuwa hatua hii itapelekea kumpata rais atakaye kuwa chaguo la asilimia kubwa ya wananchi.

Nafasi zitakazo pigiwa kura

Katika uchaguzi huu wapiga kura watamchagua rais, naibu wake, wabunge (wawakilishi na maseneta) pamoja na wajumbe wa serikali za ugatuzi (magavana wa kaunti na wawakilishi wa tarafa).

Katiba ya Kenya inataka kuwepo na uchaguzi Jumanne ya pili ya mwezi wa Agosti kila mwaka wa tano. Rais huchaguliwa kupitia mfumo ulioboreshwa wa duru mbili; ili kushinda katika duru ya kwanza, mgombea anapaswa kupata zaidi ya 50% ya kura za jumla na 25% katika kaunti zisizopungua 24.

Kwa mujibu wa IEBC Wabunge 337 wanachaguliwa kwa njia mbili; 290 huchaguliwa katika majimbo. Viti vingine 47 vinatengwa kwa ajili ya wanawake, ambao wanachaguliwa kuwakilisha kaunti 47 za Kenya. Wajumbe 67 wa baraza la Seneti wanachaguliwa kwa njia nne. Wajumbe47 wanachaguliwa katikangazi ya kaunti. Kwa utaratibu uliopo vyama vya siasa vinagawana nafasi 16 za wanawake, mbili za vijana na mbili kwa ajili ya watu wenye ulemavu kulingana na jumla ya kura walizojikusanyia.

Changamoto zinazoikabili Tume Huru ya Uchaguzi

Tume ya uchaguzi inasema kuwa inaangalia baadhi ya changamoto zilizokuwepo katika uchaguzi wa 2013, kama vile ukosefu wa elimu kwa wafanyakazi wake juu ya matumizi ya teknolojia ya kupiga kura na vituo kuchelewa kupata vifaa vya uchaguzi.

Hivi sasa tume hiyo inasema kuwa ina mfumo maaluum wa usimamizi wa uchaguzi (KIEMS) ambao kwa sasa unatumika kuthibitisha uandikishaji wa wapiga kura. Mfumo huu pia utatumika siku ya uchaguzi kuthibitisha wale wanaostahili kupiga kura, matokeo ya uchaguzi na hata usambazaji wa matokeo ya kura kwa kituo cha kitaifa cha kuhesabu kura.

Mitandao ya kijamii

Mitandao ya kijamii ina nafasi kubwa sana katika uchaguzi huu kuliko zamani.Wakenya wengi wanatumia mtandao wa Twitter na wanajulikana kama KOT (Kenyans on Twitter). Wana msukumo mkubwa katika kampeni na wanaitumia mitandao kuuza sera na ilani za uchaguzi za wale wanaowaunga mkono.

Vyama vya siasa pia vimeajiri wahamasishaji ambao wana wafuasi wengi katika mitandao ya jamii kushinikiza ujumbe wao. Pia kuna wale ambao wameajiriwakuandika na kuvipamba vyama vyao ili kusahihisha katika mitandao kampeni hasi zinazofanywa dhidi vyama hivyo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG