Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 22:39

Mugabe asherehekea miaka 90


Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe akisherehekea siku ya kuzaliwa kwake

Akipinga mapenzi wa jinsia moja, Mugabe alisema;“tumeumbwa kama wanaume na wanawake ili tuweze kuzaa watoto.Na hivyo ndivyo ilivyo."

Rais Wa Zimbabwe Robert Mugabe Jumapili alisherehekea miaka 90 ya kuzaliwa kwake mjini Harare.

Katika hotuba iliyotolewa kwa zaidi ya saa nzima, Kiongozi huyu mkongwe kabisa barani Afrika alisema hataruhusu wapenzi wa jinsia moja nchini Zimbabwe. Alisema hilo ndilo linalochangia kusambaa kwa virusi vya HIV na Ukimwi.

Mugabe alinukuliwa na vyombo vya habari akielezea kuwa; “tumeumbwa kama wanaume na wanawake ili tuweze kuzaa watoto. Na hivyo ndivyo ilivyo.”
Bw. Mugabe ambaye ametawala Zimbabwe tangu ilipopata uhuru wake mwaka wa 1980, alisema pia kuwa atapambana na ufisadi.

Matamshi yake yalifuatia kukamatwa kwa baadhi ya maafisa wa ngazi ya juu kutoka kwa shirika la ndege la kitaifa kutokana na tuhuma za ufisadi uliohusisha dola milioni 10.

Baada ya hotuba yake bwana Mugabe alikata keki kadhaa, mojawapo ikiwa na uzani wa kilo 90. Kisha wafuasi wake wakaanza kugawa zawadi ikiwemo mifugo 90 huku mfanyabiashara mmoja akimpa dola elfu 20 taslimu.

Sherehe hizo zaaminika kugharimu takriban dola milioni moja.Wanachama wa upinzani hawakuhudhuria sherehe hizo wakisema wanapinga kushindwa kwa bwana Mugabe kuokoa uchumi wa nchi unaozidi kuzorota.
XS
SM
MD
LG