Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 02:45

ZANU-PF yampa Mugabe hadi Jumatatu kujiuzulu


Zimbabwe Political Turmoil
Zimbabwe Political Turmoil

Chama kinachotawala nchini Zimbabwe, ZANU-PF, Jumapili kilimpatia rais Robert Mugabe hadi Jumatatu adhuhuri kujiuzulu kwa hiari, la sivyo kitaanza mchakato wa kumuondoa kupitia kanuni za kikatiba.

Awali, ZANU-PF kilimpokonya uongozi rais Mugabe na badala yake kumteua aliyekuwa makamu wa rais Emmerson Mnangagwa kama kiongozi mpya wa chama hicho.

Mugabe alimwachisha kazi makamu huyo wiki iliyopita. Wakati huo huo, Grace Mugabe, ambaye ni mkewe rais Mugabe, amefukuzwa kutoka kwa chama hicho, ambako alikuwa kiongozi wa tawi la wanawake.

Kiraja wa upinzani bungeni, Innocent Gonese, aliliambia shirika la habari la Associated Press, kwamba iwapo rais Mugabe hatakuwa ameachia madaraka kufikia siku ya jumanne, basi mchakato wa kumuondoa utaanza bungeni.

Jumamosi, maelfu ya Wazimbabwe walioonekana kuwa na furaha walifanya maandamano kwenye barabara za Harare na miji mingine ya nchi hiyo, huku wengine wakielekea kwa makazi rasmi ya rais Mugabe, kumshinikiza kujiuzulu.

Hata hivyo, mpwa wa rais huyo, Patrick Zhuwao, akizungumza kutoka pahali ambapo hapakutambuliwa nchini Afrika Kusini, alisema kuwa Mugabe na mkewe hawakuwa tayari kujiuzulu na kwamba walikuwa tayari kupoteza maisha yao, kwa kusimamia kile walichokiita 'usahihi wa mambo.'

XS
SM
MD
LG