Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:41

Mugabe aondolewa katika uongozi wa ZANU-PF


Wajumbe wa Kamati Kuu ya ZANU-PF katika mkutano
Wajumbe wa Kamati Kuu ya ZANU-PF katika mkutano

Chama kinachotawala Zimbabwe, ZANU-PF, Jumapili kimemfukuza Robert Mugabe kutoka katika wadhifa wake wa uongozi ndani ya chama.

Pia kimeteua aliyekuwa makamu wa rais Emmerson Mnangagwa kuchukua nafasi ya Mugabe. Mnangagwa alifukuzwa kutoka katika wadhifa wake na Mugabe wiki mbili zilizopita.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Zimbabwe, sakata hilo la Mnangawa limezua mzozo mkubwa wakati jeshi la nchi hiyo lilipochukuwa madaraka na kumzuia Mugabe 93, nyumbani kwake. Mugabe alikuwa amemteua mke wake Grace kuwa makamu wa rais.

Maelfu ya wazimbabwe waliojawa na furaha waliandamana kwenye barabara za mji wa Harare Jumamosi, wakimtaka rais Robert Mugabe kujiuzulu huku baadhi yao wakibeba mabango yaliyoandikwa 'Mugabe Must Go'.

Jeshi, ambalo limekuwa likizuia maandamano kama hayo katika siku za nyuma mjini Harare, Jumamosi lilionekana kuunga mkono waandamanaji hao, na kuwaelekeza kwenye uwanja ambako hotuba zilitolewa na wanaharakati, wanasiasa na wapiganiaji wa zamani wa ukombozi, waliomtaka rais huyo kujiuzulu.

Maandamano pia yalifanyika katika miji mingine nchini humo, wengi wakitoa wito huo huo, kwamba kiongozi huyo mkongweaondoke madarakani.

XS
SM
MD
LG