Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 17:54

Mugabe aenda Singapore kwa matibabu


Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe

Katika siku za nyuma rais huyo amekanusha kuwa anaugua.

Maafisa nchini Zimbabwe wanasema Rais Robert Mugabe amekwenda Singapore tena Alhamis kwa matibabu. Hata hivyo maafisa hao hawakuelezea rais huyo wa miaka 87 anaugua ugonjwa gani.

Bw.Mugabe alikuwa Singapore mwezi jana kwa uchunguzi wa kina wa jicho baada ya kufanyiwa upasuaji mwaka jana. Katika siku za nyuma rais huyo wa Zimbabwe amekanusha kuwa anaugua.

Jumatano, bwana Mugabe alitishia kunyakua biashara zinazomilikiwa na wageni, kulipiza kisasi vikwazo alivyowekewa yeye na washirika wake wa kisiasa na nchini Magharibi. Akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Harare Bw. Mugabe alitaja benki na makampuni yanayodhibitiwa na Uingereza.

Alisema kuna zaidi ya makampuni mia nne yanayomilikiwa na uingereza nchini Zimbabwe zikiwemo benki za Barclays na Standard Chartered. Mugabe alisema wakati umewadia wa kuchukua hatua dhidi ya makapuni hayo na kuongeza kuwa vikwazo vya nchi za magahribi ndizo zilizoduma uchumi wa nchi yake.

XS
SM
MD
LG