Wabunge wanaishiwa na muda wa kufanya mashauriano kwa mpango huo kuhusu usalama wa mpaka ambao Waripublikan, wanasema lazima wajumuishwe ili kuondoa wasiwasi wao kuhusu ufadhili wa kigeni wa migogoro huku wakiacha vipaumbele vya ndani bila kushughulikiwa.
“Jambo hili linahusu kulinda mipaka yetu ili tuweze kuwasaidia washirika wetu,” Seneta wa Ripublikan Lindsey Graham aliwaambia waandishi wa habari Alhamisi.
Graham alitoa wito kwa rais wa Marekani, Joe Biden, kutekeleza sheria zilizopo za uhamiaji, akisema yeye asingependa kurejea katika jimbo lake la South Carolina, kujieleza kwa nini anaisaidia Ukraine, Taiwan na Israeli, huku wakiwa hawajafanya chochote kulinda mpaka wao wenyewe.
Forum