Kiongozi wa walio wengi katika baraza la Seneti, Chuck Schumer, alikiri Jumatatu kwamba mazungumzo hayo yatachukua muda.
Ameongeza kusema kila mtu anajua kwamba kuna jambo linafaa kufanywa kurekebisha mfumo wetu wa uhamiaji ulioharibika, lakini hatuwezi kufanya hivyo kwa kuathiri maadili yetu.
Marekani tayari imetenga zaidi ya dola bilioni 100 kwa ajili ya silaha na kusaidia Ukraine, toka Russia, kuanzisha mashambulizi yake kamili Febuari 2022, na rais Joe Biden wa Marekani, ameliomba bunge kupitisha dola bilioni 60 nyingine.
Hata hivyo Warepublikan wameongezeka kuwa na wasiwasi wa umuhimu wa kuendelea kuisaidia Ukraine.
Forum