Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 02:05

Hosni Mubarak arudi tena mahakamani


Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak akiwa kwenye machela ndani ya chumba cha mahakama mjini Cairo, Augusti 15,2011
Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak akiwa kwenye machela ndani ya chumba cha mahakama mjini Cairo, Augusti 15,2011

Kesi ya Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak imeanza tena Jumatatu huku waandamanaji nje ya mahakama wakiwarushia mawe polisi

Kesi ya Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak imeanza tena Jumatatu ambapo mahakama moja mjini Cairo imesikiliza ushahidi kutoka kwa ofisa mmoja wa zamani wa polisi na maafisa wengine kadhaa.

Bwana Mubarak alikuwepo baada ya kuwasili akiwa kwenye machela. Nje ya mahakama majeshi ya usalama yalipambana na waandamanaji ikiwemo baadhi ambao waliwarushia mawe polisi.

Kesi hiyo haikuonyeshwa moja kwa moja kwenye televisheni kama ilivyokuwa vikao viwili vya awali ambavyo vilimuonyesha Bwana Mubarak akiwa amelala kwenye kitanda cha hospitali ndani ya chumba cha mahakama pamoja na watoto wake wawili wa kiume wakiwa pembeni yake. Jaji aliamuru kesi hiyo kutotangazwa moja kwa moja kama ilivyokuwa mwezi uliopita.

Bwana Mubaraka amekana mashtaka kwamba aliamrisha mauaji ya waandamanaji 850 wakati wa ghasia ambazo zilipelekea yeye kuondoka madarakani mwanzoni mwa mwaka huu. Pia anakabiliwa na mashtaka ya rushwa na kutumia vibaya madaraka yake.

Watoto wa kiume wa kiongozi huyo wa zamani, Alaa na Gamal wamekana mashtaka tofauti ya rushwa dhidi yao.

Bwana Mubarak anashtakiwa pamoja na waziri wa zamani wa mambo ya ndani Habib al-Adly na manaibu sita ambao wanashutumiwa kwa kutoa amri ambayo ilipelekea vifo vya waandamanaji.

Bwana Mubarak ni kiongozi wa kwanza wa kiarabu kufikishwa mahakamani tangu vuguvugu la kutaka mabadiliko ya uongozi yaliyotanda kote Afrika kaskazini na mashariki ya kati mwaka huu.

XS
SM
MD
LG