Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 07:34

Mubarak: Nitaendelea kuongoza hadi Septemba


Umati wa watu wanaopinga serikali ya Hosni Mubarak katika uwanja wa Tahrir, Cairo Feb. 10, 2011.
Umati wa watu wanaopinga serikali ya Hosni Mubarak katika uwanja wa Tahrir, Cairo Feb. 10, 2011.

Rais Hosni Mubarak hakutangaza kuondoka madarakani kama ilivyotazamiwa katika hotuba kwa taifa lake Alhamisi usiku, akisema ataendelea kuwa kiongozi mpaka uchaguzi mkuu mwezi Septemba. Alisema hata hivyo kuwa baadhi ya madaraka yake yatahamishiwa kwa makamu rais wa nchi hiyo.

Akisema kuwa uhamishaji wa madaraka kwa njia ya amani umeanza, Bwana Mubarak aligoma kukubali madai ya maelfu ya waandamanaji wanaopinga serikali ambao walingia mitaani siku 17 zilizopita wakidai kujiuzulu kwa Mubarak.

Waandamanaji katika uwanja wa Tahrir walimzomea rais wakati anahutubia, wakisema "toka, toka." Awali waandamanaji walijawa na furaha kufuatia ripoti kuwa Mubarak atatangaza kujiuzulu katika hotuba hiyo.

Ilikuwa mara ya pili katika muda wa wiki mbili Mubarak kuliambia taifa kuwa ataendelea kuwa madarakani mpaka mwezi Septemba.

Mapema Alhamisi maafisa wa jeshi waliwaambia waandamanaji kuwa rais Mubarak "atakidhi" madai yao - matamshi ambayo yalichukuliwa kama kuwa atatangaza kuondoka madarakani.

Mhadhir wa chuo kikuu cha Florida Charles Bwenge anasema inavyo onekana kuna mvutano wa kisiasa ndani ya serikali huko Misri na huwenda ndio maana Mubarak akafanay alivyo fanya kutoacha madaraka.

XS
SM
MD
LG