Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 09:51

Muasi Ongwen ajisalimisha kwa majeshi ya C.A.R


Wanajeshi wa Uganda People's Defence Force -UPDF wakifanya doria msituni kulisaka kundi la LRA
Wanajeshi wa Uganda People's Defence Force -UPDF wakifanya doria msituni kulisaka kundi la LRA

Marekani inasema kamanda mmoja wa cheo cha juu katika kundi la Lord’s Resistance Army huenda amejisalimisha mwenyewe kwa majeshi ya Marekani huko Afrika ya kati.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema Jumanne kwamba mtu huyo anayedaiwa kuwa ni Dominic Ongwen amejisalimisha huko Jamhuri ya Afrika ya kati-CAR. Washauri wa jeshi la Marekani wapo C.A.R. kusaidia jeshi la Umoja wa Afrika kulisaka kundi la LRA na viongozi wake.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Jen Psaki alisema juhudi za kutambua kikamilifu wajihi wa mshukiwa muasi zinaendelea. Alisema kama Ongwen ni kweli amejisalimisha mwenyewe, itakuwa ni pigo la kihistoria kwa muundo wa LRA.

Mwanajeshi wa Uganda katika harakati za kulisaka kundi la LRA
Mwanajeshi wa Uganda katika harakati za kulisaka kundi la LRA

Kundi la LRA linadaiwa kwa mauaji na utekaji nyara wa maelfu ya watu kote kwenye mataifa manne ya Afrika kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita. Kundi hilo lilipigana na serikali ya Uganda kwa miongo miwili kabla ya kugawanyika kwa makundi na kuwa na wapiganaji wanao hama hama ambao mara kwa mara wameshambulia na kufanya wizi katika makazi ya maeneo ya vijijini.

Marekani imetoa hadi dola milioni tano kwa taarifa zinazopelekea kukamatwa kwa Ongwen. Anatafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC yenye makao yake The Hague kwa shutuma za uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Ongwen ni mmoja wa viongozi watano wa LRA wanaotafutwa na mahakama hiyo ya ICC akiwemo kiongozi wa juu wa kundi hilo Joseph Kony.

XS
SM
MD
LG