Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 02:59

Mtu mmoja auwawa katika mlipuko Nairobi


Rais wa Kenya Mwai Kibaki

Mtu mmoja auawawa na wengine kadhaa wajeruhiwa katika mlipuko Nairobi.

Maafisa huko Kenya wanasema mtu mmoja aliuwawa na wengine 29 walijeruhiwa jumapili wakati mlipuko ulipotokea mjini Nairobi na kuchoma kituo cha mafuta.

Mashahidi wanasema mlipuko ulitokea kiasi cha saa 5 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki karibu na bara bara ya Kinyiraga mjini Nairobi. Wale waliojeruhiwa walipelekwa hospitali ambapo watu kadhaa walitibiwa kwa majeraha ya kuungua vibaya.

Maafisa hawajafahamu bado kama mlipuko huo ulikuwa ni ajali au ni makusudi.

XS
SM
MD
LG