Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 15, 2025 Local time: 15:08

Mtu aokolewa kutoka chini ya kifusi kufuatia shambulio la Russia huko Ukraine


Waokoaji wakimuondoa muathirika wa kombora la Russia katika mji wa Kharkiv, Ukraine Septemba 1, 2024. Picha na REUTERS/Yevhen Titov
Waokoaji wakimuondoa muathirika wa kombora la Russia katika mji wa Kharkiv, Ukraine Septemba 1, 2024. Picha na REUTERS/Yevhen Titov

Vikosi vya uokoaji katika mji wa Kharkiv nchini Ukraine wamempata mtu akiwa hai kutoka katika kifusi katika ukumbi wa sherehe ambao ulishambuliwa na makombora siku ya Jumapili.

Muathirika huyo aliyenusurika katika shambulio hilo alisema punde baada ya kuokolewa kuwa “anajisikia vizuri,” baada ya madaktari kumuweka katika kitanda cha wagonjwa na kumbeba mtu huyo aliyeonekana kutodhurika

Makombora ya Russia huko Kharkiv yaliwajeruhi watu zaidi ya 40 wakiwemo watoto, mamlaka zimesema.

Makombora kadhaa yalipiga eneo la maduka na ukumbi wa sherehe majira ya mchana katika mji wa mashariki.

Vikosi vya Ukraine vimeushambulia mkoa wa kusini mwa Russia la mkoa wa Belgorod siku ya Jumapili, na kujeruhi watu 11 wakiwemo watoto wawili ambao wamejeruhiwa vibaya, gavana wa mkoa huo Vyacheslav Gladkov amesema.

Gladkov, aliandika ujumbe kwenye mtandao wa Telegram, alisema wavulana wawili wanafanyiwa upasuaji baada ya kupata majeraha mabaya mmoja wao akiwa na majeraha makubwa kwenye miguu yote miwili. Madaktari wanafikiria kuwapeleka Moscow kwa ajili ya matibabu zaidi.

Shambulio limeharibu nyumba 22 makazi ya watu na nyumba binafsi nane pamoja na magari zaidi ya 20, amesema.

Shrika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha kutoka vyanzo huru juu ya idadi hiyo. Maafisa wa Ukraine hawakutoa maoni.

Forum

XS
SM
MD
LG