Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 06:28

Sudan yamuhamisha mshukiwa wa uhamiaji haramu


Sudan imemuhamisha mtu ambaye anashukiwa kuwa kiongozi wa shughuli za kuhamisha watu kuelekea Italia, Polisi wa Italia wamesema.

Raia wa Eritrea, Yehdego Mered, mwenye umri wa miaka 35, alikamatwa mjini Khartoum mwisho wa mwezi Mei.

Mered amekuwa kwenye orofdha ya watu wanaotafutwa kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa tuhuma za usafirishaji haramu wa kimataifa wa biandamu.

Taarifa iliyotolewa na polisi wa Italia ilisema kuwa Mered ni mmoja wa wasafirishaji wakuu wa binadamu na ambaye amekuwa akiendesha operesheni zake kutoka nchini Libya kupitia eneo lililo chini mwa jangwa la Sahara.

Taarifa hiyo iliendelea kusema kwamba mtuhumiwa huyo aliendesha operesheni zake sio tu barani Afrika, bali pia alikuwa akiwasiliana na walanguzi wengine nchini Italia, na kuwapasha kuhusu tarehe za boti kuwasili, ili kuwawezesha wawamiaji hao kuendelea na safari zao hadi Ulaya.

XS
SM
MD
LG