Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 12:57

Polisi waendelea na uchunguzi wa mtu waliyemkuta na silaha Marekani


Maafisa usalama wanachunguza mwenendo wa mtu ambaye alikuwa na silaha katika gari lake ambaye anasema alipanga kuhudhuria gwaride la Gay Pride jana Jumapili huko Los Angeles katika jimbo la California, Marekani.

Baada ya kupokea simu kuhusu mshukiwa, polisi waligundua uwezekano wa milipuko na shambulizi la silaha katika gari linalomilikiwa na James Howell mwenye umri wa miaka 20 kutoka Indiana.

FBI wanafanya uchunguzi juu ya suala hilo. Howell aliwaambia polisi kwamba alipanga kuhudhuria tamasha na hakuwa na mpango wa kufanya jambo lolote la kuumiza.

Polisi wanasema hakuna uhusiano wowote kati ya Howell na ufyatuaji mbaya wa mauaji ya umma kuliko yote katika historia ya Marekani ambao uliuwa watu 50 huko Orlando katika jimbo la Florida.

Maafisa wameongeza usalama baada ya ukamataji huo na gwaride lilifanyika bila ya kutokea tukio lolote baya.

XS
SM
MD
LG